BARCELONA leo wameikosa nafasi safi sana ya kuiporomosha Real Madrid kutoka kilele cha La Liga walipofungwa kwao Nou Camp Bao 1-0 Malaga.
Bao la ushindi la Malaga lilifungwa Dakika ya 7 tu kufuatia Beki wao Dani Alves kurudisha Pasi fupi kwa Kipa wake Claudio Bravo na Straika wa Malaga, Juan Miguel Jimenez Lopez, kuunasa Mpira huo na kufunga.
Mwezi Septemba, huko kwao La Rosaleda, Malaga ilifanikiwa kutoka 0-0 na Barca.
Matokeo haya yamewabakisha Vinara Real Madrid kileleni mwa La Liga wakiwa Pointi 1 mbele na Mechi moja mkononi ambayo watacheza Kesho Jumapili Ugenini na Elche.
No comments:
Post a Comment