West Ham ndio waliotangulia kwa kufunga katika Dakika ya 49 kwa Bao safi la Beki wao Cheikhou Kouyate lakini huku zikiongezwa Dakika 4 za Majeruhi, Blind aliisawazishia Man United baada ya Krosi ya Marcos Rojo kuleta kizaazaa Golini mwa West Ham.
Man United walimaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada ya Luke Shaw kupewa Kadi ya Njano ya Pili na hivyo kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu mara baada ya kusawazisha Bao.
Sare hii imewabakisha Man United Nafasi ya 4 na Jumatano Usiku watakuwa kwao Old Trafford kucheza na Burnley katika Mechi nyingine ya Ligi Kuu England.
VIKOSI:
West Ham wanaoanza: Adrian, Jenkinson, Song, Tomkins, Cresswell, Kouyate, Noble, Downing, Nolan, Valencia, Sakho
West Ham Akiba: Jarvis, O'Brien, Amalfitano, Jaaskelainen, Cole, Oxford, Lee
Manchester United wanaoanza: De Gea, Valencia, Jones, Rojo, Shaw, Blind, Rooney, Januzaj, Di Maria, van Persie, Falcao
Man United Akiba: Mata, Smalling, Ander Herrera, Fellaini, Valdes, McNair, Wilson
Kocha Van Gaal amewaambia wachezaji wake kujituma Uwanjani na kuongeza bidii ili kuondoka na pointi tatu muhimu dhidi ya West Ham United.
No comments:
Post a Comment