Mwalimu Akida (kulia) na Rolland Revocutus (katikati) wakimpongeza nahodha wao Ally Rabbi baada ya kufunga mabao matano peke yake kwenye mchezo huo wa jana
Ally Rabbi akipongezwa
Mwansasu aliyasema hayo baada ya kufanikiwa kuondoa Kenya kwenye mchezo wa raundi ya kwanza uliochezwa ufukwe wa Escape One jijini Dar es Salaam juzi na kuifunga mabao 7-6.
Tanzania kwenye mchezo wa awali uliochezwa Mombasa nchini Kenya Tanzania ilishinda mabao 5-3 hivyo imefuzu raundi ya pili kwa kuifunga Kenya jumla ya mabao 12-9 itakutana na timu ya Taifa ya Misri kati ya Machi 7, 8 na kurudiana kati ya Machi 13, 14, 2015
“Namshukuru Mungu tumeshinda mchezo wa leo lakini bado tuna safari ndefu kwani Misri ambao ndo tutacheza nao raundi ya pili ni timu nzuri hivyo tunahitaji maandalizi mazuri na sapoti ya mashabiki”, alisema Mwansasu
Endapo Tanzania itafanikiwa kuiondoa Misri itakuwa imefuzu moja kwa moja katika fainali za Mataifa ya Afrika yatakayofanyika kwenye Visiwa vya Shelisheli April mwaka huu
Kikosi cha Tanzania
Kikosi cha Kenya
Wachezaji wa akiba wa Tanzania wakifuatilia mpambano
Wachezaji wa Kenya na viongozi wao wakiwa hawaamini kuwa safari yao ya kwenda Shelisheli imeishia ufukwe wa Escape one jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment