
Sina mbavu mieee nipisheeee!!! Chicharito baada ya kuizima Atletico Madrid usiku huu!

Ilikuwa ni Usiku wa kipekee kwa Chicharito!!

Chicharito akishangilia bao lake la pekee baada ya kuifungia na kuipa Ushindi Real usiku huu dhidi ya Atletico Madria kwenye marudiano ya Klabu Bingwa Ulaya. Bao hilo limewapeleka Real Madrid Nusu Fainali ya 31 na Droo ya Nusu Fainali itachezeshwa Ijumaa ya wiki hii.

1-0 Tunasonga hatua ya Nusu Fainali sisi ni mabingwa watetezi bwana!
Javier Hernández aliwafungia bao Real Madrid dakika za majeruhi na kufanya 1-0 dhidi ya Atletico Madrid, Ni Baada ya kupewa pasi ndani ya boksi na Staa wa Real Cristiano Ronaldo na kufunga bao hilo la Ushindi. Real wamesonga hatua ya Nusu faonali kwa Ushindi wa bao la Chicharito. Mtanange huu pia Atletico Madrid walimaliza pungufu wachezaji 10 Uwanjani baada ya mwenzao Arda Turan kuoneshwa kadi njano ya pili na kuoneshwa kadi Nyekundu kwa kumchrzea rafu mbaya mchezaji wa Real Madrid Sergio Ramos.
Cristiano Ronaldo akiendesha..mpira wakati wa kipindi cha kwanza

Chicharito hoi! akishangaa kuona mpaka kipindi cha kwanza kinakatika bado 0-0, Ngoma ngumu!

Ronaldo akiachia shuti

Ronaldo tena..

Arda Turan akioneshwa kadi ya njano

Sergio Ramos kwenye patashika mpira wa kichwa!

jino kwa jino!

Arda Turan akimwangaisha Fabio wa Real

Ronaldo akijishika kichwa katika kipindi cha kwanza

Sergio Ramos chini akijiuguza katika kipindi cha kwanza.

Kikosi cha Real Madrid kilichoanza dhidi ya Atletico Madrid

Kikosi cha Atletico Madrid

Diego Semeone na Carlo Ancelotti wakisaliniana kabla ya kipute kuanza Bernabeu

Mashabiki wa Real madrid wakiwapungia Mastaa wao

VIKOSI:
Real Madrid: Casillas, Carvajal, Varane, Ramos, Coentrao, Pepe, Kroos, Isco, Rodriguez, Ronaldo, Hernandez.
Akiba: Navas, Arbeloa, Khedira, Lucas Silva, Illarmendi, Jese.
Atletico Madrid: Oblak, Juanfran, Miranda, Godin, Jesus Gamez, Tiago, Koke, Saul, Arda, Griezmann, Mandzukic.
Akiba: Moya, Siqueira, Gimenez, Raul Garcia, Gabi, Jimenez, Torres.
Refa: Felix Brych
Robo Fainali-Mechi za Marudiano
Mechi zote mbili kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku
Jumatano Aprili 22
Real Madrid vs Atletico Madrid [Santiago Bernabeu, Madrid, Spain] [0-0]
AS Monaco vs Juventus [Stade Louis II, Monaco, France] [0-1]
Wachezaji wa Atletico Madrid Joao Miranda, Antoine Griezmann na Mario Mandzukic wakipasha kwenye Uwanja wa Bernabeu usiku huu, Tayari kwa marudiano ya Robo Fainal, Mshindi kwenda Nusu Fainali

Griezmann akipasha

Juanfran nae akipasha kwenye Uwanja wa Bernabeu muda mfupi kabla ya kipute kuanza.
No comments:
Post a Comment