Manchester United walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kusawazisha Dakika ya 85 na Dakika moja baadae kupiga Bao la ushindi katika Mechi waliyoitawala kabisa.
Kipindi cha Kwanza, Man United walifunga Bao safi kupitia Ibrahimovic na Refa Mason kulikataa na Gemu kubakia 0-0 hadi Mapumziko.
Kipindi cha Pili, Dakika ya 67, bila kutegemewa, Boro walitangulia kufunga kwa Bao la Grant Leadbitter na kuelekea kumpa Msaidizi wa zamani wa Jose Mourinho, Aitor Karanka, ambae ni Meneja wa Middlesbrough, ushindi huku Kipa wa zamani wa Man United Victor Valdes akiwa nguzo yao imara akiwanyima Man United bao kadhaa za wazi.
Lakini Dakika ya 85, kazi njema ya Ibrahimovic ilimpa mwanya Anthony Martial kusawazisha na Dakika 1 baadae Krosi ya Juan Mata, alieingizwa Kipindi cha Pili, kuunganishwa kwa Kichwa na Paul Pogba na kuwapa ushindi Man United wa 2-1 wakikumbusha enzi za Sir Alex Ferguson za ushindi murua wa Dakika za mwisho hasa Leo ikiwa ni Siku ya Kuzaliwa ya Lejendari alietimiza Miaka 75 akiwepo pia Uwanjani hapo Old Trafford kushuhudia Mechi hii.
Anthony Martial (85')
Paul Pogba (86')
No comments:
Post a Comment