BUKOBA SPORTS

Saturday, December 31, 2016

CHELSEA 4 vs 2 STOKE CITY, BLUES WAENDELEZA UBABE KILELENI WAKIWEKA HISTORIA MPYA EPL!


Vinara wa Ligi Chelsea wamekwenda Pointi 9 mbele baada ya kuichapa Stoke City 4-2 na kuifikia Rekodi ya Arsenal ya kushinda Mechi 13 mfululizo za Ligi hii waliyoiweka Msimu wa 2001/02.

Bao za Chelsea hii Leo zilifungwa na Cahill, Dakika ya 34, Willian, 57 na 65, na la Diego Costa la Dakika ya 85. Bao za Stoke zilipigwa Dakika za 46 na 64 kupitia Martins Indi na Peter Crouch.

No comments:

Post a Comment