Chelsea wapo kileleni wakiwa na Pointi 46, Liverpool wanafuata wakiwa na Pointi 40 na City ni wa 3 wakiwa na Pointi 39.
Leo Chelsea watacheza mapema kwao Stamford Bridge na Stoke City na kuacha zigo kubwa kwa Liverpool na Man City kupigana baadae Usiku.
Kitu chema kwa City ni kurejea tena dimbani kwa Straika wao mkuu Sergio Aguero aliyekuwa Kifungoni kwa Mechi 4.
Lakini Klabu zote zina Majeruhi kadhaa na kwa Liverpool hao ni Grujic, Coutinho, Matip, Bogdan na Ings wakati wa City ni Kompany, Delph na Gündogan.
Kwenye Mechi kama hii iliyochezwa Anfield Msimu uliopita Last season Liverpool 3 Manchester City 0.
Nini Mameneja Wameongea?
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp: "Hii ni Gemu kubwa kwa kila Timu. Klabu 6 zinagombea Nafasi 4 au moja. Kila Gemu ni kama Fainali.”
“City wana vipaji kwenye Timu yao na Benchi lao. Kitu cha maana kwetu ni kuchezea Anfield. Ni lazima tutumie hilo!” Meneja wa Manchester City Pep Guardiola: "Wao ni Wagombea Ubingwa. Nishawahi kucheza dhidi ya Jurgen Klopp, tunajuana. Anfield itawapa matumaini makubwa!”
No comments:
Post a Comment