BUKOBA SPORTS

Monday, April 27, 2015

HAZARD NDIYE MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA PFA, HARRY KANE NI BORA KWA VIJANA!

Eden Hazard wa Chelsea amechaguliwa kuwa ndie Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA, Professional Footballers Association, ambacho ni Chama cha kutetea maslahi ya Wachezaji wa Kulipwa huko England.
Tuzo ya Mchezaji Bora Kijana wa Mwaka wa PFA imekwenda kwa Straika wa Tottenham, Harry Kane mwenye Miaka 21.
Msimu huu, Hazard, mwenye Miaka 24, amefunga Mabao 13 kwa Chelsea na kutengeneza Bao 8 katika Mechi 33 za Ligi Kuu England na kuisaidia Timu yake kuukaribia Ubingwa.
Mshindi wa Tuzo za PFA huchaguliwa kwa Kura za Wachezaji wenzake wa Kulipwa.

Hazard, ambae Msimu uliopita ndie alikuwa Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora Kijana wa PFA, alikabidhiwa Tuzo yake Jana huko Grosvenor Hotel Jijini London.
Awali Jana, Hazard alichaguliwa mmoja wa Wachezaji 6 wa Chelsea kwenye Kikosi cha PFA, cha Timu Bora ya Mwaka.
Wachezaji wengine wa Chelsea kwenye Kikosi hicho ni Mabeki Branislav Ivanovic, John Terry na Gary Cahill na Viungo Nemanja Matic pamoja na Straika Diego Costa.
Wachezaji wengine waliounda Kikosi hicho cha Wachezaji 11 ni Fulbeki wa Southampton Ryan Bertrand, Straika wa Tottenham Harry Kane, Philippe Coutinho wa Liverpool, Alexis Sanchez wa Arsenal na Golikipa wa Manchester United David De Gea. 

Eden Hazard celebrates after scoringLISTI KAMILI YA WAGOMBEA:
-MCHEZAJI BORA WA MWAKA

Diego Costa (Chelsea)
David De Gea (Manchester United)
Philippe Coutinho (Liverpool)
Eden Hazard (Chelsea)
Harry Kane (Tottenham Hotspur)
Alexis Sanchez (Arsenal)

-MCHEZAJI BORA KIJANA WA MWAKA
Thibaut Courtois (Chelsea)
Philippe Coutinho (Liverpool)
David De Gea (Manchester United)
Eden Hazard (Chelsea)
Harry Kane (Tottenham Hotspur)
Raheem Sterling (Liverpool)

No comments:

Post a Comment