BUKOBA SPORTS

Monday, April 27, 2015

FULL TIME: YANGA SC 4 vs 1 POLISI MORO, KHAMIS TAMBWE APIGA HAT-TRICK!! YANGA MABINGWA LIGI KUU VODACOM MSIMU 2014/15!!


Kocha wa Yanga, Hans Pluijm akishangilia baada ya timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara msimu wa mwaka 2015-16.

Simon Msuva (kushoto) akishangilia na Amis Tambwe baada ya Tabwe kuipatia timu yake bao la katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshida 4-1. (Picha na Francis Dande)

Mashabiki wa Yanga wakishangilia bao lililofungwa na Amis Tambwe.

Mshambuliaji Wa Yanga, Simon Msuva akimtoka beki wa Polisi Moro, Hassan Mganga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Shabiki wa Yanga akifurahia bao la pili la timu yake.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya kumalizika kwa mchezona Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.
Amis Tambwe akipokea mpira baada ya kufunga"Hat Trick"
Kocha wa Yanga, Hans Pluijm akishangilia baada ya timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.
Mashabiki wakishangilia.

Yanga hii leo wametwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Vodacom kwa Msimu wa 2014/15 baada ya kuichapa Polisi Moro Bao 4-1 katika Mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Ushindi huu umewafikisha Pointi 55 huku wakibakisha Mechi 2 kumaliza Ligi na kufuatiwa na waliokuwa Mabingwa Azam FC ambao wana Pointi 45 na wamebakisha Mechi 3.
Shujaa wa Yanga hii Leo ni Straika kutoka Burundi Amisi Tambwe aliepiga Hetitriki na Bao 1 kufungwa na anaeongoza Ufungaji Bora kwenye Ligi Simon Msuva ambae sasa amefikisha Bao 17 akifuatiwa na Amisi Tambwe mwenye Bao 14
.



MSIMAMO ULIVYO TIMU ZA JUU
1. Yanga Mechi 24 Pointi 55*
2. Azam FC Mechi 23 Pointi 45
3. Simba Mechi 24 Pointi 41
4. Mbeya City Mechi 24 Pointi 31


No comments:

Post a Comment