BUKOBA SPORTS

Saturday, April 25, 2015

KIPA WA MAN UNITED DAVID DE GEA FEDHA KUMBAKISHA OLD TRAFFORD! GUNDOGAN NA DEPAY NJIANI KUTUA MAN UNITED!

Meneja wa Manchester United Louis van Gaal amesema Manchester United imetoa ofa kubwa kwa Kipa wao David de Gea ili abakie Old Trafford.
De Gea, ambae anazidi kuwika na yumo kwenye kinyang'anyiro cha kugombea Tuzo ya PFA ya Mchezaji Bora wa Mwaka huko England, amekuwa akihusishwa mno na kurudi kwao Spain kuidakia Real Madrid.
Mwezi Januari, Van Gaal alisema anatarajia De Gea, mwenye Miaka 24, kubaki Man United ambako Mkataba wake unamalizika mwishoni mwa Msimu ujao lakini hadi sasa hajasaini Mkataba mpya wa kumbakiza kwa muda mrefu zaidi.
Akihojiwa na Wanahabari kuhusu De Gea, Van Gaal alisema: "Mie si Bosi. Nataka abaki. Lakini Mchezaji mwenyewe ndio Bosi anaweza kusema Ndio au Hapana. Itabidi mumuulize De Gea na sio mimi."
Hata hivyo, Van Gaal aliongeza: "Inabidi asaini. Tumempa Fedha nyingi!"
Kuhusu Wachezaji wapya ambao wanatarajiwa kuchukuliwa mwishoni mwa Msimu na hasa Fowadi wa Holland, Memphis Depay, Van Gaal alijibu: "Sizungumzi hili na Vyombo vya Habari!"
Hata hivyo zipo habari mpya zilizotobolewa na TV ya Sky Sports ambayo imedai Man United wako mbioni Wikiendi hii kumsaini Kiungo wa Germany anaechezea Borussia Dortmund Ilkay Gundogan kwa Dau la Pauni Milioni 21.5.

No comments:

Post a Comment