Kuelekea Mechi ya Jumapili Uwanjani Emirates ambapo Arsenal itacheza na Chelsea, Jose Mourinho, Meneja wa Chelsea, amesema Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal, si mpinzani wake.
Mechi hii inazikutanisha Chelsea, ambao ni Vinara wa Ligi, na Arsenal, iliyo Nafasi ya Pili na Pointi 10 nyuma ya Chelsea huku Nafasi ya 3 inashikwa na Manchester United walio Pointi 11 nyuma ya Chelsea.
Ikiwa Chelsea wataifunga Arsenal Jumapili basi Mechi yao inayofuata hapo Jumatano Ugenini na Leicester City ushindi utawapa Ubingwa huku wakibakiwa na Mechi 4 mkononi.
Akipooza mvuto wa Wanahabari kuhusu uhasama kati yake na Wenger, Mourinho alisema: "Kwangu mimi yeye si mpinzani wangu, yeye ni Meneja wa Klabu kubwa katika Mji huo huo ambao nafanya kazi na kuishi. Klabu yake ni kubwa yenye malengo kama sisi. Kwa sababu hiyo upinzani unakuwepo lakini kwangu si tofauti kama nilivyokuwa Inter Milan dhidi ya Meneja wa AC Milan au Real Madrid na Atletico Madrid!"
Nae Wenger alikataa kabisa kugusia uhusiano wa yeye na Mourinho hasa baada ya Mechi yao ya mwishoi kukutana huko Stamford Bridge kutaka kukunjana na badala yake akaomba Mashabiki wa Arsenal wamheshimu Cesc Fabregas ambae atarejea Emirates kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na Chelsea kutoka Barcelona mwanzoni mwa Msimu.
Kabla kujiunga na Barcelona Mwaka 2011, Fabregas aliichezea Arsenal kwa Miaka 8.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
Jumamosi Aprili 25
14:45 Southampton vs Tottenham
17:00 Burnley vs Leicester
17:00 Crystal Palace vs Hull
17:00 Newcastle vs Swansea
17:00 QPR vs West Ham
17:00 Stoke vs Sunderland
17:00 West Brom vs Liverpool
19:30 Man City vs Aston Villa
Jumapili Aprili 26
15:30 Everton vs Man United
18:00 Arsenal vs Chelsea
No comments:
Post a Comment