BUKOBA SPORTS

Thursday, April 30, 2015

SERIE A: TEVEZ NI HATARI SANA AFUNGA BAO 2, WAKIIBUKA NA USHINDI WA 3-2 DHIDI FIORENTINA....SASA JUVE WABAKISHA POINTI 1 KUNYAKUWA UBINGWA!


Mabingwa WAtetezi wa Italy Juventus Jana waliibwaga Fiorentina Bao 3-2 na kubakisha Pointi 1 tu kutwaa Ubingwa wa Serie A kwa mara ya 4 mfululizo.
Jana Juve, wakiwa kwao Juventus Stadium Mjini Turin, walitoka nyuma kwa Bao la Penati ya Rodriguez ya Dakika ya 33 na kusawazisha Dakika ya 36 kwa Bao la Fernando Llorente na Carlos Tevez kupiga Bao la Pili Dakika ya 46.
Tevez tena aliipeleka Juve Bao 3-1 mbele katika Dakika ya 70 baada ya Gonzalo Rodriguez kukosa Penati ya Dakika ya 67.
Bao la Pili la Fiorentina lilifungwa na Josip Ilicic katika Dakika ya 90.
Juve, ambao wako Pointi 14 mbele ya Timu ya Pili Lazio huku Mechi zimebaki 5, wataweza kutwaa Ubingwa Jumamosi ikiwa watapata Sare ya Ugenini wakicheza Ugenini na Sampdoria.
Juve wana Rekodi nzuri dhidi ya Lazio hivyo hata Sare kwenye Mechi hiyo na Sampdoria inawatosha hata kama Lazio watashinda Mechi zao zote zilizobaki na kuikamata Juve ikiwa Mabingwa hao watapoteza Mechi zote zao zilizobaki.

No comments:

Post a Comment