BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 22, 2015

USIKU HUU UEFA CHAMPIONS LEAGUE: REAL MADRID vs ATLETICO MADRID, CRISTIANO RONALDO KUONGOZA JAHAZI LISIZAME!

Atletico Madrid, chini ya Kocha Diego Simeone, hawajafungwa katika Mechi 6 dhidi ya Jirani zao Real Madrid ambao ndio Mabingwa wa UEFA CHAMPIONS LIGI, Ubingwa ambao waliutwaa baada ya kuitandika Atletico Bao 4-1 huko Lisbon, Ureno Mwezi Mei Mwaka Jana.Tangu wakati huo Atletico imekuwa kidedea mbele ya Real kwa kuichapa 1-0 Uwanjani Vicente Calderon na kutwaa Kombe la Spain la Super Cup kwa Jumla ya Bao 2-1 baada ya Sare ya 1-1 huko Santiago Bernabeu.
Wiki 3 baadae, Atletico ikaifunga tena Real 1-0 ndani ya Nyumba ya Real, Santiago Bernabeu, katika Mechi ya La Liga na kisha kuitoa Jumla ya Bao 4-2 katika Mechi mbili za Copa del Rey Mwezi Januari ambazo Atleti ilishinda 2-0 kwao na Sare 2-2.
Baada ya hiyo kikaja kichapo cha 4-0 alichopewa Real kwenye La Liga Mwezi Februari na Wiki iliyopita ndio ikaja Sare ya 0-0 huko Vicente Calderon katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI.

Na ili kutetea Taji lao la Ulaya, ni lazima Real washinde kwani wakiruhusu Sare yeyote ya Magoli Atletico ndio watatinga Nusu Fainali kwa Bao za Ugenini.
Lakini Real wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa na upungufu wa Wachezaji wao muhimu kina Marcelo, ambae yuko Kifungoni, na Kiungo Luka Modric na Fowadi Gareth Bale ambao ni Majeruhi, huku kukiwa na hatihati kama Karim Benzema atacheza kwani ana maumivu ya Enka.
Nao Atletico huenda wakamkosa Fowadi wao hatari Mario Mandzukic ambae anauguza Enka na akikosekana basi Mtoto wa Nyumbani Fernando Torres atavaa Jezi.


Robo Fainali-Mechi za Marudiano
Mechi zote mbili kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku

Jumatano Aprili 22
Real Madrid vs Atletico Madrid [Santiago Bernabeu, Madrid, Spain] [0-0]
AS Monaco vs Juventus [Stade Louis II, Monaco, France] [0-1]

No comments:

Post a Comment