BUKOBA SPORTS

Friday, May 1, 2015

KIPIGO CHAMBWETUSHA KOCHA NIGEL KWA MWANDISHI WA HABARI, AOMBA MSAMAHA MARA MOJA!

Kocha wa Leicester City Nigel Pearson
Meneja wa Leicester City Nigel Pearson ameomba radhi kwa mwandishi wa habari aliyemtukana.
Pearson ameomba radhi kwa Ian Baker aliyemtolea maneno machafu baada ya kumuliza swali kuhusu madhaifu ya wachezaji wake yaliyosababisha timu kuboronga msimu mzima.
"Namuomba msamaha Ian ,Nilitaka kufanya hivyo mara moja mbele ya camera sikua na furaha kwa sababu ya kupoteza mchezo"alieleza kwenye mkutano wa waandishi wa habari.
Na kwa upande wake Ian Baker amekubali kupokea msamaha huo baada kocha huyo kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment