BUKOBA SPORTS

Friday, July 31, 2015

FA COMMUNITY SHIELD: CHELSEA vs ARSENAL JUMAPILI HII, NANI KUIBUKA KIDEDEA!

 NGAO YA Jamii huko England ndio Mechi ya fungua dimba Msimu mpya na hushindaniwa kati ya Mabingwa Watetezi wa England na waliobeba FA CUP na safari hii Mabingwa Chelsea wataivaa Arsenal ambao walitwaa FA CUP Msimu uliopita.
Wakati Arsenal wakitinga kwenye mtanange huo wakiwa na matokeo mazuri kwenye Mechi zao za kabla ya Msimu za kugombea Barclays Asia Trophy huko Singapore na Emirates Cup Uwanjani kwao Emirates Jijini London na kubeba Makombe yote, Mabingwa Chelsea wao hawajashinda hata Mechi moja, ndani ya Dakika 90, katika Mechi zao za matayarisho.
Katika Mechi hizo, Arsenal walipata ushindi mkubwa pale walipoichapa Lyon ya France 6-0 Uwanjani Emirates na pia kuitwanga Everton 3-1 huko Singapore.
Katika Mechi zao 4 za majaribio, Arsenal wameona nyavu mara 14 na kufungwa mara 1 tu huku Kipa Mkongwe, Petr Cech, waliemnunua toka Chelsea aking’ara.
Cech anaweza kukutana na Timu yake ya zamani kwa mara ya kwanza Jumapili hii ikiwa atapangwa wakati Arsenal wakisaka kutwaa Ngao ya Jamii kwa mara ya pili mfululizo kwa mara ya kwanza tangu 1999.
Wakati Arsenal wakibembea kuelekea Mechi hii ya Ngao ya Jamii ambayo Msimu uliopita waliitwanga Manchester City 3-0 na kuibeba, Chelsea wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa hawajashinda ndani ya Dakika 90 baada ya kuhitaji Tombola ya Penati kuzibwaga PSG na Barcelona kufuatia kuchapwa 4-2 na New York Red Bulls kwenye Mashindano ya International Champions Cup huko Marekani.
Mbali ya hayo, Chelsea pia hawana Rekodi nzuri ya kutwaa Nagao ya Jamii baada ya kuitwaa mara 4, mara ya mwisho ikiwa 2009, wakati Arsenal wameibeba mara 13 wakipitwa tu na Liverpool waliotwaa mara 15 na vinara Manchester United ambayo imeichukua mara 20.

Mourinho akiteta jambo na Terry na  Fabregas pamoja na wengine

Wachezaji wa Chelsea wamejifua leo Ijumaa tayari kwa kipute jumapili
Chelsea kukutana na Washindi wa  FA Cup  Arsenal kwenye  Community Shield  huko  Wembley siku ya jumapili

No comments:

Post a Comment