BUKOBA SPORTS

Sunday, January 31, 2016

KAGERA SUGAR YAIFANYIA KITU MBAYA MBEYA CITY, YAICHAPA BAO 2-0 LEO SHINYANGA!

Wafungaji ni Paul Ngwai na Babu Ally, Mabao yote yamefungwa kipindi cha pili.
Kambarage, Shinyanga, Kagera Sugar iliitandika Mbeya City Bao 2-0 kwa Bao za 63 na 79 zilizofungwa na Paulo Ngaliona na Babu Ali.
VPL itaendelea tena Jumatano kwa Mechi 7 ambapo Vinara wa Ligi na Mabingwa Watetezi, Yanga, wapo huko Sokoine Mbeya kucheza na Tanzania Prisons wakisaka kufuta machungu ya kuchapwa 2-0 na Coastal Union Juzi huko Tanga.
Simba, ambao Juzi waliizaba African Sports 4-0 ukiwa ni mwendelezo wa mwanzo mzuri wa Kocha wao mpya kutoka Uganda Jackson Mayanja, wao wapo Dar es Salaam Uwanja wa Taifa kuivaa Timu kigaga Mgambo JKT.
 

No comments:

Post a Comment