Barcelona wamepaa kileleni mwa La Liga baada ya kuwachapa Mtu 9 Atletico Madrid 2-1 katika Mechi iliyochezwa Nou Camp hii Leo.
Atletico walitangulia kufunga katika Dakika ya 10 kwa Bao la Koke na Barca kusawazisha Dakika ya 30 kupitia Lionel Messi na Dakika 8 baadae Luis Suarez akaipa Barca Bao la Pili na la ushindi.
Atletico walibaki Mtu 10 katika Dakika ya 44 Filipe Luis kupewa Kadi Nyekundu kwa kumchezea Rafu mbaya Messi.
Dakika ya 65 Diego Godin alipewa Kadi ya Njano ya Pili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu na kuiacha Timu yake Atletico ikiwa Mtu 9 na Bao 2-1 nyuma.
Bao hizo zilidumu hadi mwisho wa Mechi na kuifanya Barca izidi kuongoza La Liga ikiwa na Pointi 51 kwa Mechi 21 ikifuatiwa na Atletico wenye Pointi 48 kwa Mechi 22 na wa 3 ni Real Madrid wenye Pointi 44 kwa Mechi 21.
No comments:
Post a Comment