BUKOBA SPORTS

Thursday, February 25, 2016

LEO USIKU WA EUROPA, MAN UNITED, LIVERPOOL, SPURS ZOTE DIMBANI ENGLAND, NANI KUIBUKA KIDEDEA?

LEO ni Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI za Marudiano na Timu zote 3 za England zinazocheza Mashindano hayo ziko Viwanja vya Nyumbani kusaka ushindi ili kusonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Man United wapo kwao Old Trafford huku Wiki iliyopita huko Denmark, wakichapwa 2-1 na FC Midtjylland, na hivyo Leo ni ushindi tu ndio utawakomboa.
Huko Anfield, Liverpool wanatinga kurudiana na Augsburg ya Germany ambayo walitoka nayo 0-0 huko Germany Wiki iliyopita na hivyo ushindi au Sare yeyote ya Magoli ni faida kwao.
Nako huko White Hart Lane Jijini London, Wenyeji Tottenham Hotspur watacheza na Fiorentina ya Italy ambayo walitoka nayo 1-1 na sasa ushindi au Sare ya 0-0 itawafaa Spurs.

Lakini Sare yeyote ya kuanzia 2-2 kwenda juu itawatupa nje Spurs.

No comments:

Post a Comment