Mtoto wa Afghanistan aliepata umaarufu Duniani baada ya kupigwa Picha akivaa Jezi iliyotengenezwa kienyeji kwa Mfuko wa Plastiki wa Rangi za Argentina na Jina la Messi huku pia ikiwa na Namba 10 sasa amekabidhiwa Jezi halisi na Lionel Messi mwenyewe ambayo ameisaini.
Mtoto huyo mwenye Miaka Mitano aitwae Murtaza Ahmadi anampenda mno Messi lakini Familia yake ya Kimaskini inayoishi Jimbo la Ghazni Jirani na Mji Mkuu wa Afghanistan, Kabul, Nchi ambayo ina misukosuko ya vita, haina uwezo wa kununua Jezi Orijino ya Staa huyo wa Argentina
Kaka wa Murtaza, Homayoun, mwenye Miaka 15, aliamua kumtengenezea Mdogo wake Jezi ya Argentina kutoka Mfuko wa Plastiki na kuiandika Jina la Messi na Namba 10 kwa Peni na kisha kuiposti Picha yake kwenye Mtandao wa Facebook Mwezi uliopita.
Picha hiyo ilizagaa mno Dunia nzima na kuwa maarufu kupindukia.
Wiki kadhaa zilizopita, Jorge Messi, Baba Mzazi wa Lionel Messi, alisema Lionel Messi anajua kuhusu Picha hizo na anataka kufanya kitu kwa ajili ya Shabiki wake huyo Mtoto wa Afghanistan ikiwa pamoja na kukutana nae.
Mtoto huyo mbali ya kupewa Jezi halisi, pia amepewa Mpira.
Habari hizi zimethibitishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto Tawi la Afghanistan, UNICEF, ambalo liliposti Twitter iliyosema: “Murtaza ana kitu halisi. Leo Messi amesaidia kuifanya ndoto yake iwe kweli na kumkabidhi Jezi iliyosainiwa na Mpira.” Messi ni mmoja wa Mabalozi wa UNICEF.
No comments:
Post a Comment