BUKOBA SPORTS

Thursday, February 25, 2016

VAN GAAL AWATAKA WACHEZAJI WA MANCHESTER UNITED KUCHEZA SOKA SAFI NA "UCHU" ILI WAWEZE KUJIZOLEA POINTI!

Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal amewataka wachezaji wake kuwa na ''uchu'' katika mechi ya kombe la Europa dhidi ya FC Midtylland.
United iko nyuma kwa mabao 2-1 na itaikaribisha timu hiyo ya Denmark nyumbani.
Na alipulizwa kile alichokihitaji kutoka kwa timu yake ,Van Gaal alijibu: Tamaa,njaa mara nyingi mimi hutumia neno ''uchu''.
Ufanisi katika ligi ya Europa ndio matumaini makubwa ya Manchester United kufuzu katika ligi ya vilabu
Baada ya kupoteza 2-1 kwa Sunderland katika ligi ya Uingereza,mashetani hao wekundu wana alama sita chini ya kilabu ya nne katika jedwali la ligi ya Uingereza.

Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 64 anakabiliwa na madai kwamba huenda kazi yake ikachukuliwa na aliyekuwa mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho na amekuwa akikosolewa na mashabiki.

No comments:

Post a Comment