José Mourinho ndie Meneja mpya wa Manchester United kwa Msimu wa 2016/17 baada ya kusaini Mkataba wa Miaka Mitatu ambao pia unaweza kumuweka hadi Mwaka 2020.
José, Raia wa Ureno mwenye Miaka 53 na ambae ametwaa Makombe 22 tangu 2003, amefundisha Klabu kadhaa kubwaa Ulaya na kutwaa Mtaji katika Nchi 4 tofauti (Portugal, England, Italy na Spain) ikiwa pamoja na kutwaa UEFA CHAMPIONS LIGI, mara 2 akiwa na FC Porto 2004 na Inter Milan 2010.
Akitangaza rasmi uteuzi huu, Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United Ed Woodward, alisema: “Jose ni Meneja Bora kabisa kwenye Gemu hivi sasa. Ametwaa Mataji na kuhamasisha Wachezaji katika Nchi kadhaa Ulaya na pia anaijua Ligi Kuu England nje ndani ambako ametwaa Ubingwa mara 3! Namkaribisha Manchester United!”
Nae José Mourinho amesema: "Kuwa Meneja wa Manchester United ni heshima spesho katika Gemu. Ni Klabu inayojulikana na inayopendwa Dunia nzima. Kuna kitu cha ajabu na mapenzi ambacho Klabu nyingine yeyote hawana!”
Aliongeza: “Siku zote nimekuwa na mvuto mkubwa na Old Trafford, na huu umekuwa ni Uwanja wenye kumbukumbu muhimu kwangu na pia Mashabiki wao tuko vyema. Sasa nina hamu kubwa kuwa Meneja wao na kufurahia sapoti yao kwa Miaka ijayo!”
Zlatan Ibrahimovic kutua nae Old Trafford
AKIONGEA na MUTV, Kituo cha TV cha Manchester United mara baada ya kusaini Mkataba wa Miaka mitatu kuwa Meneja mpya, Jose Mourinho ameserma atafanya kila awezalo kuirejesha Man United kileleni mwa Soka la Dunia.
Mourinho amesema: “Najisikia safi. Nimepata heshima na nasikia fahari, nipo hapa kufanya kazi na nangojea kwa hamu Julai 7 kuingia Uwanjani!”
Aliongeza: “Nadhani hili limekuja wakati muafaka kwa sababu Manchester United ni Klabu kubwa kabisa!”
“Tunaweza kuitazama Klabu yetu kwa namna mbili. Moja ni Miaka Mitatu iliyopita na nyingine ni Historia yake. Mie napenda kusahau Miaka Mitatu iliyopita na kutia mkazo kwenye Historian ya hii Klabu kubwa ambayo iko mikononi mwangu!”
Mourinho alidokeza kuwa moyoni aliipenda Man United kwa muda mrefu sana na kila akienda Old Trafford akizungumza Klabu zake humuona anazipinga.
Mourinho ameeleza: “Nakumbuka tulishinda Old Trafford na Real Madrid [UEFA CHAMPIONS LIGI 2012/13 Raundi ya Mtoano ya Timu 16] na nikasema Timu bora ilifungwa na Real Madrid hawakufurahia hilo!”
No comments:
Post a Comment