Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mungereza (kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 50 kwa mshindi wa Airtel Music Stars Tanzania 2016, Melisa John, mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo. Melisa amejishindia shilingi milion50 pamoja na kupata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Airtel Trace Music Stars Afrika.
mshindi wa Airtel Music Stars Tanzania 2016, Melisa John akipongezwa na mama yake baada ya kuibuka mshindi nakupata kitita cha shilingi milioni 50.
Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Bi Gabriel Kaisi (kulia) akimkabithi Nandi Charles mfano wa hundi ya shilingi milioni 5 mara baada ya kuibuka mshindi wa pili wa shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania, katika shindano hilo Melisa John aliibuka kuwa mshindi wa kwanza.
wanavyoimba ili kupata mshindi wa shindano hilo kwa Tanzania
Mshindi wa tatu wa shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania Salim Mlindila akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 2 kutoka kwa Meneja wa kampuni ya Tabasamu, Lucy Ngongoseke.
mshindi wa Airtel Music Stars Tanzania 2016, Melisa John, akiongea mara baada ya kutangazwa mshindi na kukabithiwa mfano wa hundi ya shilingi miliioni 50. Kulia ni mama yake Melisa John,na kushoto nao MC wa fainali hizo.
Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Tanzania 2016, Melisa John, akiimba mara baada ya kutangazwa mshindi katika fainali za shindano la Airtel Trace Music Stars zilizofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam. Melisa amejishindia shilingi milioni 50 pamoja na kupata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Airtel Trace Music Stars Afrika. Mshindi wa pili wa mashindano hayo ni Nandi Charles na Watatu ni Salim Mlindila
Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga akitumbuiza wakati wa fainali za shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaama, wakati wa fainali hizo, Mayunga pia alizindua wimbo wake wa video aliomshirikisha mwimbaji wa Marekani Akon ujulikanao kama “ Please don’t go away”
Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga akitumbuiza wakati wa fainali za shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaama, wakati wa fainali hizo, Mayunga pia alizindua wimbo wake wa video aliomshirikisha mwimbaji wa Marekani Akon ujulikanao kama “ Please don’t go away”
Majaji wa shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania, Luciano Gadie Tsere(kushoto) na Tony Joett wakifatilia kwa makini washiriki
Baadhi wa waalikwa waliojitokeza kushuhudia shindano la Airtel Trace music Stars wakiwa katika picha wakati wa koktaili kabla ya shindano hilo kuanza
Washiriki walioingia katika tano bora ya shindano la Airtel Trace Music Stars wakiimba wimbo wa pamoja wakati wa finali za shindano hilo lililofanyika ukumbi wa JINCC jijini Dar es Saalam.
Wageni waalikwa mbalimbali wakifatilia na kuwashangilia washiriki wa shindano la Airtel Trace Music Stars wakiwa Jukwaani huku wakirekodikumbukumbu mbalimbali kupitia simu zao za mkononi
Wageni waalikwa mbalimbali wakifatilia na kuwashangilia washiriki wa shindano la Airtel Trace Music Stars wakiwa Jukwaani huku wakirekodikumbukumbu mbalimbali kupitia simu zao za mkononi.
No comments:
Post a Comment