MANCHESTER UNITED wametwaa FA CUP kwa mara ya kwanza tangu 2004 baada ya Jesse Lingard kufunga Bao la ushindi katika Dakika za Nyongeza 30 huku wakiwa Mtu 10 walipoifunga Crystal Palace 2-1 Uwanjani Wembley Jijini London.
Palace walitangulia kufunga Dakika ya 79 kwa Bao la Jason Puncheon lakini Sekunde 175 baadae Kepteni Wayne Rooney aliichambua Palace na kumimina Krosi ambayo Fellaini aliemshushia Juan Mata aliefunga.
Hadi Dakika 90 Bao zilibaki 1-1 na Gemu kwenda Dakika za Nyongeza 30.
Dakika ya 110, Jesse Lingard alieingizwa Dakika ya 90 kumbadili Juan Mata alifunga Bao la ushindi baada ya kazi nzuri ya Rooney.
-Hii ni Mechi ya Fainali ya 135 ya FA CUP.
-Fainali hii ni kama Marudio ya Fainali ya Mwaka 1990 ambayo Manchester United waliifunga Crystal Palace 1-0 baada ya Mechi ya kwanza kwisha Sare 3-3.
-Hii ni mara ya Pili kwa Palace kutinga Fainali wakati kwa Man United ni Fainali ya 18 na wameshinda 11 kati ya hizo wakipitwa tu na Arsenal walioshinda Fainali 12
-Mara ya mwisho kwa Man United kutwaa FA CUP ni Mwaka 2004 walipoifunga Timu ya Daraja la Kwanza Millwall 3-0.
Hili ni Taji la kwanza kwa Meneja Van Gaal kutwaa Taji lake la kwanza akiwa na Man United na pia kuipa Klabu hiyo Kombe la kwanza tangu Sir Alex Ferguson astaafu Mei 2013 ingawa mwanzoni mwa Msimu wa 2013/14, wakiwa chini ya David Moyes, walibeba Ngao ya Jamii walipoibwaga Man City.
Manchester United XI: De Gea, Valencia, Smalling, Blind, Rojo, Carrick, Mata, Fellaini, Rooney, Martial, Rashford
Man Utd subs: Jones, Young, Romero, Ander Herrera, Schneiderlin, Lingard, Darmian
Crystal Palace starting XI: Hennessey, Ward, Dann, Delaney, Souare, Jedinak, Cabaye, Zaha, McArthur, Bolasie, Wickham
Crystal Palace subs: Speroni, Mariappa, Gayle, Adebayor, Sako, Kelly, Puncheon
No comments:
Post a Comment