Jumatano CBF, Shirikisho la Soka la Brazil, lilimteua Tite, mwenye Miaka 55, kuchukua nafasi ya Dunga alietimuliwa hivi Majuzi baada ya Brazil kushindwa kusonga kutoka Hatua ya Makundi ya Copa America Centenario walipofungwa 1-0 kwa Bao la utata na Peru huko USA.
Tite, ambae Jina lake kamili ni Adenor Leonardo Bacchi, ataacha kuifundisha Klabu ya huko Mjini Sao Paulo, Brazil, Corinthians, ambayo ametwaa nayo Mataji kadhaa, ili kushika hatamu Timu ya Taifa ya Brazil.
Brazil ndio Wenyeji wa Michezo ya Olimpiki itakayochezwa Nchini humo Mjini Rio de Janeiro kuanzia Agosti 5 hadi 21.
Pele alisema: “Tite ni mtu anaeaminika.”
Kuhusu Dunga, Pele alisema Dunga hakuwa na makossa kwani hakuwa na muda kuitayarisha Timu na kufungwa ndio Soka.
No comments:
Post a Comment