Kadhalika Rais Jamal Malinzi amempongeza Clement Sanga kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti baada ya kupata kura 1,428 wakati mpinzani wake Titus Osoro alipata kura 80. Kura 1,508 zilipigwa katika nafasi ya kuwania makamu mwenyekiti.
Wajumbe waliochaguliwa ni Omary Said (1,069), Siza Lyimo (1,027), Salum Mkemi (894), Thobius Lingalangala (889), Ayoub Nyenzi ((889), Samwel Lukumay (818), Hussein Nyika (770) na Hashim Abdallah (727.
Katika salamu hizo za pongezi, Rais Jamal Malinzi pia amewapongeza wanachama wa Young Africans kwa kufanya uchaguzi wa amani na utulivu.
Kutokana na hali hiyo, Rais Jamal Malinzi amewataka uongozi huo wa Young Africans kufungua ukurasa mpya wa kuendesha klabu hiyo na kuiletea mafanikio klabu hiyo kongwe na maarufu katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kati hasa wakati huu ambako Young Africans inashiriki hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC).
No comments:
Post a Comment