Akizungumza na gazeti hili Shime alisema timu yake ameiandaa vyakutosha kwani imepata mechi za kimataifa za kirafiki hali iliyomwezesha kukisuka vema kikosi hicho.
“Naamini kwa maandalizi haya tutasonga mbele kwenye hatua inayofuata na vijana wana ari ya kwenda Madgascar 2017 kwenye fainali za mashindano haya”, alisema Shime.
Serengeti Boys iliingia kambini Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo huo wa Jumapili na marudiano ni Shelisheli Julai 2, 2016, endapo itafuzu hatua hii itakutana na timu ya Vijana ya Afrika Kusini.
Naye nahodha wa timu hiyo, Issa Makamba amesema wapo tayari kupambana na anaamini ushindi ni wao huku akiwataka mashabiki kuja kuwashangilia.
No comments:
Post a Comment