BUKOBA SPORTS

Thursday, July 21, 2016

ENGLAND WAONGEZA MAKALI MSIMU MPYA, WAONGEZA KANUNI MPYA – LUGHA CHAFU, ISHARA MBAYA NI REDI KADI!

KUANZIA Msimu huu mpya wa 2016/17 unaoanza Agosti 13 kwa Ligi Kuu England, Mamlaka husika huko England zimeafiki mabadiliko ya Kanuni ambapo Wachezaji watalambwa Kadi Nyekundu kwa kutumia Lugha chafu au kutoa ishara mbaya kwa Waamuzi wa Mechi.
Sambamba na hilo, pia Mabenchi ya Ufundi ya Timu Uwanjani yatadhibitiwa kwa Kanuni hizi mpya.
Kwa Misimu Mitano iliyopita, kwenye Ligi Kuu England, hajawahi kutolewa nje Mchezaji kwa kutumia Lugha chafu dhidi ya Marefa.
Mwenyekiti wa Ligi Kuu England, Richard Scudamore, amesema wamekuwa wakipata wasiwasi baada ya Wachezaji kudhihirika wakitumia Lugha chafu na ishara mbaya kwa Marefa.

KADI YA NJANO
- Makosa yanayoweza kumpa Mchezaji Kadi:
-Tabia ya wazi mbaya kwa Waamuzi
-Kuhamaki kwa ghadhabu baada ya Refa kutoa uamuzi
-Kumkabili Refa uso kwa uso
-Kumkimbilia Refa kubisha uamuzi
-Lugha chafu au ishara mbaya kwa Refa
-Kumgusa Refa
-Kadi ya Njano kwa Mchezaji Mmoja endapo Wachezaji Wawili au zaidi watamzonga Refa
KADI NYEKUNDU – Kanuni Mpya:
-Kumkabili Refa na kutumia Lugha chafu au ishara mbaya kwa Refa au Wasaidizi wake
-Kumgusa Refa kwa ugomvi au ubishi
**Sheria hizi Mpya zitatumika kwa Ligi zote za England

No comments:

Post a Comment