
Kesho Alhamisi, Bodi ya FA, Chama cha Soka England, kitakaa kumpitisha kama Meneja wao mpya kuchukua nafasi ya Roy Hodgson aliemaliza Mkataba wake Majuzi tu baada ya kwisha Fainali za EURO 2016 na England kutolewa kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na ‘vibonde’ Iceland.
Kwenye mchakato wa uteuzi wa wadhifa huu, Allardyce, maarufu kama Big Sam, alichuana vikali na Meneja wa Hull City Steve Bruce aliewahi kuichezea Manchester United.
Mapema hii Leo, Mtendaji Mkuu wa FA, Martin Glenn, alithibitisha kuwa Bodi ya Watu 12 ya FA itajulishwa rasmi kuhusu mchakato wa uteuzi wa Meneja wa Timu ya Taifa ili itoe uamuzi kwenye Kikao chao cha Alhamisi.
Wiki iliyopita, aliewahi kuwa Meneja wa Man United, Sir Alex Ferguson, mwenye asili ya Scotland na ambae ndie Meneja mwenye mafanikio makubwa katika Historia ya Uingereza, aliwapasulia wazi England kuwa Mtu pekee anaefaa wadhifa wa Meneja wa England kwa sasa ni Sam Allardyce
No comments:
Post a Comment