WINGA wa Portugal Nani, ambae Jumatano Usiku ataiwakilisha Nchi yake kwenye Nusu Fainali ya EURO 2016 dhidi ya Wales, amejiunga na Valencia ya Spain kutoka Fenerbahce ya Uturuki na kusaini Mkataba wa Miaka Mitatu. Valencia imethibitisha Uhamisho huu bila kutoa idadi ya Ada ya Uhamisho baada ya kutoa Taarifa kwenye Tovuti yao ikisema Luis Carlos Almeida – 'Nani' – Mchezaji wa Kimataifa wa Portugal atakuwa na wao kwa Miaka Mitatu.
Valencia imefanikiwa kumchukua Nani, mwenye Miaka 29, baada ya kushinda majaribio ya Klabu ya England Stoke City iliyomtaka Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United na Sporting Lisbon.
No comments:
Post a Comment