Nao Swansea City wapo njiani kumsaini tena Straika wao wa zamani Wilfried Bony, mwenye Miaka 27, ambae sasa yupo Man City.
Nae Straika wa Everton, Romelo Lukaku, mwenye Miaka 23, anawania kurejea tena Chelsea.
Winga wa Marseille Georges-Kevin N'Koudou, 21, anakaribia kukamilisha Uhamisho kwenda Tottenham na yeye anamfuatia Straika wa Netherlands Vincent Janssen, 22, ambae tayari yupo White Hart Lane.
Meneja pya wa Sunderland manager David Moyes anataka kumsaini Straika Will Keane, 23, kutoka Manchester United kwa Dau la Pauni Milioni 6.5.
Wakati huo huo, Wapinzani Manchester United na Manchester City wametumbukia kwenye mvutano wa kumuwania Straika Chipukizi wa Brazil Gabriel Jesus, 19.
No comments:
Post a Comment