BUKOBA SPORTS

Friday, August 12, 2016

EPL LIGI YENYE PURUKUSHANI KUANZA MSIMU MPYA 2016/2017 LEO, NANI ATAWIKA?

Jose Mourinho.
Pep Guardiola.
MSIMU MPYA wa Soka wa Ligi Kuu huko England unaanza Jumamosi Saa 8 na Nusu Mchana huko Kingston upon Hull, KCOM Stadimu, kwa Timu iliyopanda Daraja Hull City kuwakaribisha Mabingwa wa England Leicester City lakini macho yapo kwa nini kitajiri kwa Mameneja wapya wenye Majina makubwa kwenye Ligi hiyo.
Safari hii Ligi hii haina tena Jina la Mdhamini na itajulikana rasmi kama Ligi Kuu tofauti na Msimu uliopita ilipoitwa Barclays Premier League kutokana na udhamini wa Barclays.

Baada ya Mechi hiyo, Saa 11 Jioni, zitafuata Mechi 5 nyingine na Saa 1 na Nusu Usiku, kuchezwa Mechi ya mwisho ya Siku hiyo huko Etihad kati ya Manchester City na Sunderland.

Jumapili ziko Mechi 2 na ya mwanzo ni huko Uwanjani Dean Court wakati Wenyeji AFC Bournemouth, watakapo wakaribisha Manchester United na kufuatia mtanange mkali huko London Uwanja Emirates kati ya Arsenal na Liverpool.

Raundi ya Kwanza ya Ligi Kuu England itakamilika Jumatatu Usiku huko Stamford Bridge kati ya Chelsea na West Ham.
Mvuto mkubwa huko England ni kuona kama Leicester wanaweza kutetea Taji lao, kitu ambacho kimefutwa na Wachambuzi karibu wote -kama si wote huko England.

Pia kuona nini Mameneja wapya wenye Majina makubwa Duniani watakifanya ukianzia Jose Mourinho wa Man United, Antonio Conte wa Chelsea, Pep Guardiola wa Man City, Ronaldo Koeman wa Everton, David Moyes wa Sunderland, Claude Puel waSouthampton na Walter Mazzarri wa Watford.

Antonio Conte Arsene Wenger Jurgen Klopp Claudio Ranieri
RATIBA: LIGI KUU ENGLAND
Msimu Mpya 2016/17
Jumamosi Agosti 13

1430 Hull City v Leicester City
1700 Burnley v Swansea City
1700 Crystal Palace v West Bromwich Albion
1700 Everton v Tottenham Hotspur
1700 Middlesbrough v Stoke City
1700 Southampton v Watford
1930 Manchester City v Sunderland

Jumapili Agosti 15

1530 A.F.C. Bournemouth v Manchester United
1800 Arsenal v Liverpool

Jumatatu Agosti 16
2200 Chelsea v West Ham United

No comments:

Post a Comment