Lionel Messi amefuta uamuzi wake wa kustaafu kuichezea Timu ya Taifa ya Argentina,
Messi, mwenye Miaka 29, aliamua kustaafu kuichezea Nchi yaka mara tu baada ya kutolewa na Chile kwenye Fainali ya Copa America Mwezi Juni huko USA.
Kwenye Fainali hiyo, Messi alikosa Penati kwenye Mikwaju ya Penalti Tano Tano na kuifanya Argentina ishindwe kutwaa Taji katika Fainali za Mashindano makubwa Manne katika Miaka 9.
Messi, ambae ameifungia Argentina Bao 55 katika Mechi 133, ametwaa Taji 1 tu akiichezea Nchi yake na hilo ni Medali ya Dhahabu kwenye Fainali za Michezo ya Olimpiki ya Mwaka 2008.
Jana Messi aliteuliwa kuwemo kwenye Kikosi cha Argentina cha kucheza Mechi za Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini za kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia zitakazochezwa dhidi ya Uruguay na Venezeula mwanzoni mwa Septemba.
Mara baada ya kugeuza uamuzi wake wa kustaafu, Messi ameripotiwa kusema amerejea tena kuichezea Argentina kwa sababu ya mapenzi kwa Nchi yake na Jezi ya Argentina.
Messi ametajwa kwenye Kikosi hichon cha Argentina ambacho kitakuwa chini ya Meneja Mpya Edgardo Bauza na Wachezaji kutoka England ambao wamo humo ni Watatu wa Man City Sergio Aguero, Pablo Zabaleta na Nicolas Otamendi, Wawili wa Manchester United Sergio Romero na Marcos Rojo, Ramiro Funes Mori wa Everton na Erik Lamela wa Tottenham.
Messi yumo humo Kikosini pamoja na mwenzake wa Klabu yao FC Barcelona ya Spain Javier Mascherano wakifanya Jumla ya Wachezaji 27 Kikosini.

No comments:
Post a Comment