Mbali ya kuzungumzia kuhusu Kikosi chake kwa ajili ya Mechi hiyo, Mourinho pia aliwajibu Meneja wa Arsenal Arsene Wenger na wa Liverpool Jurgen Klopp ambao waliponda jitihada za Man United kumsaini Kiungo wa Juventus Paul Pogba kwa Dau la Rekodi ya Dunia la Pauni Milioni 100.
Akigusia kuwa atamsaini Kiungo Bora ndani ya Siku kadhaa zijazo, Mourinho ameeleza: “Tuna Wachezaji 22. Tuakuwa na 23. Pogba ni Mchezaji wa Juve hadi ambapo rasmi sio. Soko linafungwa Agosti 31. Tunajaribu kukamilisha kabla Agosti 14!”
Kuhusu maendeleo yake na Mazoezi ya Kikosi chake, Mourinho amesema kuwa Timu yake ni tofauti na ile ya Meneja aliepita Louis van Gaal.
Kuhusu Ngao ya Jamii, Mourinho amesema: “Nadhani hii ni spesho waliokuwepo Msimu uliopita, ina maana kwao. Kucheza kwenye Ngao ya Jamii ni lazima uwe Bingwa au umetwaa FA CUP. Na wao walishinda FA CUP. Ni wazi tutajaribu kubeba Ngao ya Jamii!”
Pia Mourinho alieleza mipango yake ya kutumia Wachezaji wote 6 wa Akiba wanaoruhusiwa kucheza Mechi hiyo ya Ngao ya Jamii ili kuwapa nafasi Wachezaji zaidi Kikosini mwake.
Kwa upande wa Majeruhi, Mourinho ametoboa kuwa Chris Smalling na Tim Fosu-Mensah sasa wapo fiti na wapo mazoezini.
No comments:
Post a Comment