BUKOBA SPORTS

Sunday, August 14, 2016

Rais Magufuli amwambia Mjomba anazimikia kibao cha Sizonje


Anacheeeka! Muimbaji mashuhuri wa mashairi nchini, Mrisho Mpoto au Mjomba akisalimiana na Rais Dr Pombe Magufuli kwenye Uwana wa Ndege jjjini Dar es Salaam jana. Kulia kwa mjomba ni Katibu Mkuu wa CCM Ibrahim Kinana.
Na Mwandishi Wetu
RAIS Dr John Pombe Magufuli amefurahishwa na kibao cha muimbaji mashuhuri wa mashahiri nchini, Mrisho Mpoto cha Sizonje, ambacho kinazugumzia hali halisi ya nchi na mambo mengine, imeelezwa.

Rais Magufuli alikutana ana kwa ana na muimbaji huyo jana kwenye Uwanja wa Ndege wazamani jijini Dar es Salaam wakati akirejea kutoka katika ziara ya kikazi katika mikoa mbalimbali nchini ukiwemo Mwanza, ambako alihutubia juzi kwenye viwanja vya Furahisha.


Mrisho Mpoto au Mjmba akicheza ngoma wakati akisubiri kutua kwa Rais Dr Pombe Magufuli jana akitokea Mwanza.

Mpoto alisema jana kuwa alikwenda Uwanja wa Ndege akiwa na kundi lake la ngoma lililoko chini ya Mjomba Theatre, ambapo alikuwa akipiga ngoma, kucheza na nyoka na sarakasi, na Rais baada ya kuteremka katika ndege, alianza kutembelea vikundi vya burudani na moja kwa moja alikwenda kwa Mjomba.


Baada ya kushuhudia kidogo maonesho ya Mjomba, Magufuli alimuita msanii huyo na kusalimiana naye kabla ya kuanza kuzungnumza naye na hapo ndipo alipomueleza kuwa, kibao cha Sizonje ndio chaguo lake kubwa, kwani anakipenda sana.



Kwa mujibu wa Mpoto, Rais alisema kuwa Sizonje ndio kibao chake bora kabisa, ambapo alimsifu Mjomba kwa kibao hicho, ambacho kimejaa mafumbo mengi yanayowafanya watu kuwa na mawazo tofauti.

Alisema Rais Magufuli alimuambia anaipenda nyimbo yake ya mwisho, ambayo ni Sizonje na akuyatamka baadhi ya maneno yaliyomo katika kibao hicho.


“Nasikiliza sana nyimbo zako, ila huu wa Sizonje nimeuelewa sana na nausikiliza kila siku,… mwanzo nilipata tabu sana kuuelewa, lakini sasa hivi, aaah nimeuelewa vibaya mno, “alisema Mjomba akimkariri Rais Maufuli.

Mpoto anajulikana kwa vibao vyake, ambapo aliwahi kuimba kibao cha Mjomba, ambacho wengi walitafsiri kuwa alimuimba Rais wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete, lakini alipoulizwa mjomba ni nani, Mpoto alisema: Ni kaka yake mama.”


Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baadae uwanjani hapo, Mpoto alisema kuwa amefarijika sana kwa maneno ya busara kutoka kwa Rais, inanitia moyo sana kujua kuwa Rais ni shabiki wangu mkubwa na yeye mwenyewe kwa maneno yake amesema huwa anasikiliza nyimbo zangu akiwa Ikulu, “alisema Mjomba.

No comments:

Post a Comment