MAN UNITED wameifunga Zorya Luhansk ya Ukraine 1-0 katika Mechi yao ya pili ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI.
Ushindi huu umeiweka Man United kwenye Reli baada ya kupoteza Mechi yao ya kwanza ya Kundi A huko Rotterdam walipofungwa na Feyenoord 1-0.
Bao la ushindi la Man United lilifungwa Dakika ya 69 kwa Kichwa na Zlatan Ibrahimovic kufuatia Krosi ya Fulbeki Fosu-Mensah kuunganishwa fyongo na Wayne Rooney na Mpira kudunda juu na Ibrahimovi kuumalizia.
Bao hilo lilikuja Dakika 2 tu baada ya Rooney kuingizwa Uwanjani kumbadili Jesse Lingard.
Kwenye Mechi nyingine ya Kundi A iliyochezwa huko Uturuki, Fenerbahce iliitungua Feyenoord 1-0.
Mechi inayofuata kwa Man United ni Oktoba 20 na Fenerbahce Uwanjani Old Trafford.
No comments:
Post a Comment