BUKOBA SPORTS

Tuesday, September 6, 2016

LA LIGA: RONALDO KUREJEA REAL JUMAMOSI BERNABEU KUKIPIGA DHIDI YA OSASUNA

Cristiano Ronaldo hajacheza Mechi yeyote tangu Julai 10 alipoumia kwenye Fainali ya EURO 2016 huko Paris awakati Nchi yake Portugal ikiifunga France 1-0 na kutwaa Ubingwa wa Ulaya na yeye kucheza Dakika chache za mwanzo na kuumizwa lakini Jumamosi hii huenda akarejea tena Uwanjani kwa mara ya kwanza baada ya kupona.
Msimu huu mpya Ronaldo, ambae ndie Mchezaji Bora Barani Ulaya, hajacheza hata Mechi moja ya Klabu yake Real Madrid na alirejea Mazoezini baada ya Real kutwaa UEFA SUPER CUP walipoibwaga Sevilla mapema Agosti na pia kuzikosa Mechi mbili za La Liga ambazo zote Real walishinda.
Mechi inayofuata kwa Real ni Jumamosi Uwanjani kwao Santiago Bernabeu kwenye La Liga watakapocheza na Osasuna lakini Kocha wa Real Zinedine Zidane huenda akapanga Kikosi mchanganyiko huku akiwa na jicho moja kwenye Mechi inayofuata ya UEFA CHAMPIONS LIGI watakapocheza Jumatano Septemba 14 tena wakiwa Nyumbani Santiago Bernabeu na Sporting Lisbon ikiwa ni Mechi yao ya kwanza kabisa ya Kundi lao ya Mashindano hayo makubwa kabisa kwa Klabu Barani Ulaya ambayo wao ndio Mabingwa Watetezi.
Huenda Zidane akampa muda Ronaldo Uwanjani ili kumjenga polepole baada ya hivi karibuni kuzidisha kasi ya Mazoezi baada ya kupona Goti lake.
Kwenye La Liga, Real, Barca na Las Palmas ndizo Timu pekee zenye Pointi 6 baada ya kushinda Mechi zao zote 2 za kwanza za Msimu mpya na Ligi hiyo kusimama kwa Wiki 2 kupisha Mechi za Kimataifa.

LA LIGA
Ratiba: 

Ijumaa Septemba 9
2145 Real Sociedad v RCD Espanyol

Jumamosi Septemba 10
1400 Celta de Vigo v Atletico de Madrid
1700 Real Madrid CF v Osasuna
1915 Malaga CF v Villarreal CF
1915 Sevilla FC v Las Palmas
2130 FC Barcelona v Deportivo Alaves

Jumapili Septemba 11
1300 Sporting Gijon v CD Leganes
1700 Valencia C.F v Real Betis
1915 Granada CF v SD Eibar

2130 Deportivo La Coruna v Athletic de Bilbao

No comments:

Post a Comment