BUKOBA SPORTS

Tuesday, September 6, 2016

ULAYA U-21: MARCUS RASHFORD AICHEZEA ENGLAND U-21 KWA MARA YA KWANZA NA KUPIGA HAT-TRICK

ENGLAND U-21, Kikosi cha Vijana wa chini ya Miaka 21, sasa wanahitaji ushindi wa Mechi 1 tu ili kutinga Fainali za Mashindano ya Ulaya kwa Vijana wa U-21 baada ya Leo kuinyuka Norway 6-1 huko Colchester kwenye Mechi ya Kundi la 9 huku Marcus Rashford akipiga Bao 3.
England, wakiwa chini ya Meneja Gareth Southgate, Leo walimtumia Marcus Rashford, Kijana wa Man United mwenye Miaka 18, kwa mara ya kwanza kwenye Kikosi hicho baada ya Meneja wa England Sam Allardyce kuridhia aende huko badala ya Kikosi cha Kwanza.
Leo hii Rashford alijibu hilo kwa kupiga Bao 3 moja likiwa la Penati walipoishindilia Norway 6-1 licha ya wapinzani hao kuwa na Kijana Staa wa Real Madrid Martin Odegaard.
JE WAJUA?
-MARCUS RASHFORD:
-HUPIGA BAO KILA MECHI YAKE YA KWANZA AKICHEZEA TIMU KWA MARA YA KWANZA!
-Mechi zake za kwanza kwa Man United kwenye Ligi Kuu England na EUROPA LIGI alifunga.
-Mechi yake ya kwanza kwa Kikosi cha Kwanza cha England alifunga.
-Hii Mechi yake ya kwanza kwa England U-21 amefunga.

Bao nyingine za England zilifungwa na Lewis Baker, Ruben Loftus-Cheek na Nathaniel Chalobah.
Bao pekee la Norway lilifungwa na Ghayas Zahid.
Sasa England wamebakisha Mechi 2 kwenye Kundi la 9 na wanahitaji Pointi 3 tu kutinga Fainali Mwakani huko Poland.

VIKOSI VILIVYOANZA:
England:
Gunn, Iorfa, Targett, Chalobah, Chambers, Hause, Baker, Ward-Prowse, Rashford, Loftus-Cheek, Redmond.
Akiba: Wildsmith, Holding, Hayden, Galloway, Gray, Watmore, Akpom.

Norway: Rossbach, Haraldseid, Jenssen, Grogaard, Fossum, Sorloth, Odegaard, Berge, Daehli, El Younoussi, Selnaes.
Akiba: Dyngeland, Trondsen, Zahid, Rosted, Thorsby, Meling, Espejord.

No comments:

Post a Comment