BUKOBA SPORTS

Saturday, September 10, 2016

FULL TOME: MANCHESTER UNITED 1 vs 2 MANCHESTER CITY

MARA baada ya Jana Manchester City kuifunga Manchester United 2-1 kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England Uwanjani Old Trafford, Mameneja wa Timu zote walitoa maoni yao na pia Refa wa zamani kujitumbukiza na kudai Man United walistahili Penati. PEP GUARDIOLA AMTETEA KIPA WAKE MPYA ‘BOMU’!
BOSI wa Manchester City Pep Guardiola amemtetea Kipa wake Claudio Bravo licha ya kufanya makossa mengi kwenye ushindi wao dhidi ya Manchester United.
Hiyo ilikuwa Mechi ya kwanza kwa Bravo ambae alinunuliwa kutoka Barcelona kumbadili Joe Hart alieenda kwa Mkopo huko Torino Nchini Italy.

Wakiwa wanaongoza 2-0, Bravo alifanya kosa alipoitokea Frikiki ya Wayne Rooney na kuitema na Mpira kumkukta Zlatan Ibrahimovic aliefunga Bao kwa Man United.
Pia Bravo alimkwatua Rooney baada ya kuleta manjonjo Golini na kuupoteza Mpira kwenye tukio ambalo Wadau wengi wanadai alipaswa kupewa Kadi Nyekundu na Man United kupewa Penati.

Hata hivyo Guardiola amesema: “Tulicheza vizuri Kipindi cha Kwanza kwa sababu ya Bravo. Napenda Makipa wanaoshambulia Mpira!”

MOURINHO – TULISTAHILI PENATI 2!
MENEJA wa Manchester United Jose Mourinho anaamini Kipa wa City Claudio Bravo alistahili kupewa Kadi Nyekundu na Man United kupewa Penati baada ya kumwangusha Wayne Rooney ndani ya Boksi.
Pia, Mourinho amedai walipaswa pia kupewa Penati baada ya Beki wa City Nicolas Otamendi kuunawa Mpira.
Matukio yote hayo mawili yalipetwa na Refa Mark Clattenburg.
Mourinho alisema: “Mark alifanya makosa mawili. Claudi Bravo ni Penati na Kadi Nyekundu. Ingekuwa Mchezaji wangu kafanya hilo katikati ya Uwanja, Marouane au Rooney, ni Kadi Nyekundu na Frikiki!”

“Lile la pili Otamendi alishika Mpira. Baadhi ya Wachambuzi watasema hapana mkono ulikuwa nyuma lakini Otamendi alijua anachokifanya!”

REFA WA ZAMANI – MAN UNITED WALISTAHILI PENATI!
Refa wa zamani wa EPL Mark Halsey amesema Manchester United walipaswa kupewa Penati baada ya Kipa Claudio Bravo kumuangusha Wayne Rooney.
Pia Refa huyo amesema Bravo pia alipaswa kupewa Kadi Nyekundu kwa tukio hilo.
Lakini Refa Halsey amemtetea Refa Mark Clattenburg kwa kudai pengine hakuona vizuri tukio lenyewe kutokana na pale alipokuwepo lakini alisema Refa Msaidizi, Simon Bennett, alikuwa sehemu nzuri na alipaswa kumshauri Refa.

Wachambuzi wengi huko England wameunga mkono maoni haya na pia kuhoji uhalali wa Bao la Pili la City kwani Mfungaji Kelechi Iheanacho alionekani kuwa Ofsaidi wakati akifunga.

Kwenye Mechi hiyo, Man United walifanikiwa kusawazisha kwa Shuti la Marcus Rashford kumparaza Ibrahimovic na kutinga lakini Waamuzi hao waliamua Ibrahimovic alikuwa Ofsaidi.
Manchester United and Manchester City
VIKOSI:
Manchester United starting XI:
De Gea, Valencia, Bailly, Blind, Shaw, Pogba, Fellaini, Mkhitaryan, Rooney, Lingard, Ibrahimovic
Man Utd subs: Mata, Martial, Smalling, Rashford, Romero, Ander Herrera, Schneiderlin
Manchester City starting XI: Bravo, Sagna, Stones, Otamendi, Kolarov, De Bruyne, Fernandinho, Silva, Sterling, Iheanacho, Nolito
Man City subs: Zabaleta, Fernando, Caballero, Jesus Navas, Sane, Clichy, Garcia

No comments:

Post a Comment