WAKATI Dunia ya Soka ikisubiri kwa hamu Dabi ya Manchester itakayochezwa Jumamosi hii Uwanjani Old Trafford kati ya Mahasimu Manchester United na Manchester United huku kukiwa na shauku ya ziada ya kuwaona Mameneja wapya wa Klabu hizo, Jose Mourinho na Pep Guardiola, wakikwaana kwa mara nyingine, Mourinho ametoa tahadhari kubwa. Wawili hao walikuwa na upinzani uliojaa vituko na bashasha kubwa huko Spain walipoongoza Timu pinzani wakati Mourinho akiwa Real na Guardiola akiwa Barcelona.
Lakini, kabla ya wote kuwa Makocha Viongozi, Wawili hao walikuwa Timu moja Barcelona, Mourinho akiwa mmoja wa Jopo la Makocha na Guardiola akiwa Mchezaji na kisha kuanza Ukocha.
Lakini Mourinho amesema kwenye La Liga wasiwasi wake mkubwa ulikuwa kwa Samaki mmoja mkubwa tu lakini England kuna Papa kila kona.
“Kwa hali kama hiyo, kukwaruzana kibinafsi kunaeleweka kwani huweza kubadilisha mambo!”
No comments:
Post a Comment