BUKOBA SPORTS

Tuesday, September 6, 2016

RATIBA VPL JUMATANO: MABINGWA YANGA WAKO MTWARA NA NDANDA, SIMBA TAIFA NA RUVU SHOOTING, AZAM IPO MBEYA!

VPL
Ratiba
Jumatano Septemba 7

Simba v Ruvu Shooting
Ndanda FC v Yanga
Tanzania Prisons v Azam FC 

MABINGWA wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Yanga hii Leo wapo safarini kuelekea Mtwara ili kesho wacheze Mechi yao ya pili ya Ligi hiyo dhidi ya Ndanda FC.
Yanga wamecheza Mechi moja tu ya VPL Msimu huu walipoichapa African Lyon na baadae kukamilisha Ratiba yao ya Makundi ya Mashindano ya CAF.ya Kombe la Shirikisho.
Mechi nyingine za Jumatano zinahusu Viigogo wengine wa Dar es Salaam, Simba na Azam FC, wakicheza Mechi zao za 3 kwa Simba kuwepo Jijini Dar es Salaam kucheza na Ruvu Shooting na Azam FC kuwa Ugenini huko Mbeya kucheza na Tanzania Prisons.
Katika Mechi zao 2 zilizopita zote Simba na Azam FC zilishinda 1 na kutoka Sare 1.
Kwenye Mechi hii na Ndanda FC ambao hadi sasa wamecheza Mechi 2 za VPL na kufungwa zote na Simba na Mtibwa Sugar, Yanga itawakosa Wachezaji wao kadhaa.
Kikosi cha Yanga cha Wachezaji 20 chini ya Kocha Hans van Pluij kilichosafiri kwa Basi kwenda Mtwara hakinao Kipa Deogratius Munishi 'Dida' aliefiwa na Baba yake na Majeruhi Pato Ngonyani, Malimi Busungu na Geofrey Mwashuiya.
Wengine ambao hawamo Kikosini ni Mapro wao Vincent Bossou aliekuwa na Timu ya Taifa ya Togo na Haruna Niyonzima aliekuwa na Timu ya Taifa ya Rwanda kushiriki Mechi za kufuzu Fainali za AFCON 2017 na bado kurejea.
Hata hivyo Kocha Pluijm amesema nia yao ni kushinda Mechi hii na ile ya Jumamosi Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam dhidi ya Majimaji FC.
Nae Kocha wa Ndanda FC Hamimu Mawazo amesema watapigana ili kuepuka kipigo cha 3 mfululizo kwenye VPL. 


KIKOSI CHA YANGA KILICHOSAFIRI:
MAKIPA:
Ally Mustafa ' Barthez', Beno Kokulanya
MABEKI: Juma Abdul, Hassan Kessy, Mwinyi Haji Mngwali, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Kevin Yondani, Andrew Vincent 'Dante', Nadir Haroub ' Cannavaro'
VIUNGO: Said Juma 'Makapu', Thaban Kamusoko, Simon Msuva, Deus Kaseke, Obrey Chirwa, Yusuf Mhilu
MAFOWADI: Donald Ngoma, Matheo Anthony, Amisi Tambwe

No comments:

Post a Comment