BAADA
ya mapumziko ya siku ya jana yaliyotolewa na kocha Kinnah Phiri
kufuatia safari ndefu ya saa nyingi kutoka kanda ya ziwa, kikosi cha
Mbeya City fc leo kimeanza mazoezi rasmi kujiweka sawa kwa ajili ya
mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Azam Fc uliopangwa
kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa siku ya jumamosi.
Akizungumza
na mbeyacityfc.com mapema leo afisa habari wa City, Dismas Ten
amesema kuwa nyota wote 30 ikiwa ni pamoja na 25 waliokuwa nje ya jiji
la Mbeya kwa takribani wiki tatu kwa ajili ya michezo ya mwanzo wa
msimu wamejumuika kwenye mazoezi ya leo kwenye uwanja wa Sokoine kwa
ajili ya matayarisho ya mchezo huo wa mwishoni mwa juma.
“Tumeanza
mazoezi leo, baada ya mapumziko ya siku ya jana,nyota wetu wote wapo
ikiwa ni pamoja na wale ambao hawakusafiri na timu kwenda Mwanza na
Shinyanga kwenye michezo mitatu ya Mwanzo wa msimu ambayo
tuliikamilisha kwa kushinda miwili na suluhu moja,limekuwa ni jambo
jema kwetu kwa sababu morari imeongezeka kikosini na kila mmoja yuko
tayari kwa mchezo wa mwishomi mwa juma” alisema.
Akiendelea
zaidi Ten alisema kuwa huu ni msimu ambao City imejipanga kuvunja
rekodi zote ambazo ilikuwa haijawahi kuzifikia tangu ilipopanda daraja
misimu mitatu iliyopita.
“Huu
ni msimu ambao kwetu utakuwa na kumbukumbu nzuri kwa sababu tumejipanga
kufuta ‘madeni’ yote tuliyokuwa nayo, tangu tumepanda daraja tulikuwa
hatukuwahi kuongoza ligi hili sasa limeshakwisha,tunasubiri kuvunja
rekodi ya kutokuzifunga Yanga na Azam fc jambo ambalo tuna amini
tunalianza wikiendi hii” alitamba.
Geoffrey
Mlawa, mazoezini leo, alipokuwa akijaribu kufanya mazoezi mepesi baadae
ripoti ta daktari imesema haweza kucheza mchezo wa jumamosi dhidi ya
Azam Fc kwa sababu bado ni majeruhi. |
No comments:
Post a Comment