BUKOBA SPORTS

Saturday, September 17, 2016

SIMBA YAWEKA KISHOKA KIELENI MWA LIGI KUU TANZANIA BARA, YAILAZA AZAM KWA BAO 1-0 UWANJA WA UHURU LEO

Kipa wa Timu ya Azam FC "Wanalambalamba", Aeshi Manula akiwa chini huku Mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo akijiandaa kushangilia baada ya Kipa huyo kupitwa na mpira uliopigwa vizuri kabisa na Mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya (hayupo pichani) na kuingia moja kwa moja wavuni na kuifanya timu hiyo kujipatia bao la kuongoza. Mchezo huo ambao ulikuwa ni wenye kasi na wakuvutia huku timu zote zikishambuliana kwa zamu, umemalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam huku Timu ya Simba ikiondoka uwanjani hapo ikiwa kifua mbele kwa ushindi wa bao 1-0.

No comments:

Post a Comment