Loic Remy amerejeshwa Klabuni kwake Chelsea Siku 9 tu baada ya kuwa kwa Mkopo huko Crystal Palace bila kucheza hata Mechi moja baada ya kuumia.
Reny, Raia wa Ufaransa mwenye Miaka 29, aliumia Pajani Mazoezini Majuzi Jumatatu na sasa amerejeshwa Klabuni kwake Chelsea kupata matibabu zaidi.
Palace imethibitisha tukio hili na kusema atakuwa nje kwa Wiki kadhaa.
Meneja wa Palace, Alan Pardew, amesema: “Kwa bahati mbaya Remy aliumia Mazoezini Jumatatu. Si vibaya sana lakini Wikiendi hii hawezi kucheza na sijui atakuwa nje kwa muda gani hadi vipimo vikamilike.”
Remy alijiunga na Chelsea Mwaka 2014 na kufunga Bao 8 katika Mechi 32. Hadi sasa Palace wamecheza Mechi 3 za Ligi Kuu England na kuambua Pointi 1 tu na Jumamosi wapo Ugenini kucheza na Middlesbrough.
Mapema Leo Palace walimsaini Kiungo wa zamani wa Arsenal Mathieu Flamini ambae ni Mchezaji Huru na kufikisha idadi ya Wachezaji wao wapya kwa Msimu huu kuwa Watano na wengine ni Andros Townsend, Steve Mandanda, James Tomkins, Christian Benteke na huyu Loic Remy.
LIGI KUU ENGLANDRATIBA
Jumamosi Septemba 10
1430 Man United v Man City
1700 Arsenal v Southampton
1700 Bournemouth v West Brom
1700 Burnley v Hull
1700 Middlesbrough v Crystal Palace
1700 Stoke v Tottenham
1700 West Ham v Watford
1930 Liverpool v Leicester
Jumapili Septemba 11
1800 Swansea v Chelsea
Jumatatu Septemba 12
2200 Sunderland v Everton

No comments:
Post a Comment