BUKOBA SPORTS

Monday, September 12, 2016

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AUNGANA NA WAISLAMU KATIKA SWALA YA IDD EL HAJI VIWANJA VYA MWEMBE YANGA, TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, (kushoto), na Sheikh Ponda Issa Ponda, wakiomba dua wakati wa swala ya Idd El Haji kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam leo Septemba 12, 2016. (PICHA NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID)

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Kassim Majaliwa, amewataka waumini wa dini ya Kiislamu kuitumia sikukuu hii ya Idd el Haji kutenda mema na kuungana na waumini wengine katika kudumisha amani ya nchi yetu.
Waziri Mkuu akiyasema hayo leo Septemba 12, 2016, kwenye ibada ya sala ya Idd el Haji iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam ambapo miongoni mw masheikh maarufu walihudhuria ibada hiyo ni pamoja na Sheikh Shariff, Sheikh Nurdin Kishki,(mwenyeji wa hadhara), Sheikh Ponda Issa Ponda na Sheikh Rajab Katimba.
“Kwa niaba ya serikali yenu, nawatakia sikukuu njema, na ninaomba kuwasilisha salamu za upendo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, pamona na Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan, na niwaombe ndugu zangu muitumie sikukuu hii kudumisha amani na upendo.” Alisema Waziri Mkuu.
Waziri M,uu pia alitumia fusa hiyo kuwataka waumini wa dini ya Kiislamu kote nchini, kuwaombea wananchi wa mkoa wa Kagera waliopatwa na maafa ya tetemeko la ardhi lililosababisha vifo.
Waziri Mkuu ambaye alihudhuria ibada ya kuaga miili ya watu 16 kwenye uwanja wa michezo wa Kaitaba mjini Bukoba, mkoani Kagera Jumapili Septemba 11, 2016, alisema kwa sasa kuna majeruhi zaidi ya 100 ambao bado wanapatiwa matibabu. Tetemeko hilo lilillopelekea uharibifu mkubwa wa nyumba lilitokea Jumamosi alasiri Septemba 10, 2016.
Naye mwenyeji wa Ibada hiyo Sheikh Nurdin Kishki, alimshukuru Waziri Mkuu kwa kuungana na waumini wa dini ya Kiislamu wa Wilaya ya Temeke, katika swala hiyo ya Idd. “Nduhgu zangu napenda nimshukuru Waziri wetu Mkuu kwa kutoka Oysterbay hadi kufika huku Temeke kuungana nasi katika kutekeleza swala hii ya Idd El Haji, mwenyezimungu amjalie heri na busara katika uongozi wake,” Alsiema Sheikh Kishki.

Sheikh Shariff akiongoza Swala ya Idd El Haji viwanja vya Mwembe Yanga , Temeke jijini Dar es Salaam

Sheikh Shariff akiongoza Swala ya Idd El Haji viwanja vya Mwembe Yanga , Temeke jijini Dar es Salaam

Muumini wa Kiislamu akiomba dua

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipeana mikono na Sheikh Ponda Issa Ponda, mara baada ya swala hiyo

Waziri Mkuu, akiteta jambo na sheikh Ponda

Waziri Mku, akiwa katika picha ya pamoja na Sheikh Shariff, (kushoto), na Sheikh Nurdin Kishki

Waumini wa Kiislamu wakiwa kwenye swala

Waumini wa Kiislamu, wakiomba dua





Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Masheikh na viongozi wa serikali mara baada ya swala hiyo

Sheikh Nurdin Kishki, akisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa swala ya Idd El Haji viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam

Sheikh Nurdin Kishki, kiwahutubia waumini wa dini ya Kiislamu kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga, wakati wa swala hiyo

Watoto hawa wa Kiislamu, wakionyesha furaha baada ya kushiriki swala ya Idd El Haji, (Mlulu Khalfan (kushoto) na mdogo wake Kuugara.

Waziri Mkuu akiwaaga Waislamu baada ya swala hiyo

No comments:

Post a Comment