BUKOBA SPORTS

Tuesday, January 17, 2017

LOUIS VAN GAAL ASTAAFU SOKA

Meneja wa zamani wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Netherlands Louis van Gaal ameamua kustaafu Ukocha baada ya kuwemo kwenye kibarua hicho kwa Miaka 26.

Van Gaal, mwenye Miaka 65, amekuwa hana kazi tangu atimuliwe na Man United Mwezi Mei 2016 mara tu baada ya kuiwezesha Klabu hiyo kutwaa FA CUP. 
Habari za kustaafu kwa Van Gaal zimechomoza kwenye Gazeti la huko Netherlands, De Telegraaf, ambalo lilimnukuu akisema: “Nilidhani nitaacha nilipotoka Man United, kisha nikasema ngoja nipumzike lakini sasa naona sitarejea tena Ukocha!”

Uamuzi huo umekuja mara tu baada ya kupokea Tuzo ya Utumishi uliotukuka toka kwa Serikali ya Netherland.

Mbali ya Man United, Van Gaal pia aliwahi kuwa na Klabu za Ajax, Barcelona, Bayern Munich na AZ.

VAN GAAL – Tuzo kubwa Maishani mwake:
Ubingwa:
Ajax (1993-94, 1994-95, 1995-96), Barcelona (1997-98, 1998-99), AZ Alkmaar (2008-09), Bayern Munich (2009-10)
UEFA CHAMPIONS LIGI: Ajax (1994-95)
Uefa Cup: Ajax (1991-92)
FA Cup:
Manchester United (2015-16)

No comments:

Post a Comment