Mechi hii imekuja Siku 2 tu tangu Mlipuko wa Jijini Manchester ulioua Watu 22 na tukio hili litaifanya Man United kuvaa Utepe Mweusi Mkononi ikiwa ni ishara ya Msiba.
Pia, Uwanjani, kabla Mechi kuanza, kila Mtu atasimama Dakika 1 kimya kuomboleza.
Ajax wanatinga kwenye Fainali ya Ulaya kwa mara ya kwanza tangu 1996.
Akiongelea Fainali hii, Kocha wa Ajax Peter Bosz amesema Man United itapambana na staili yao ya mashambulizi ya haraka na mfululizo.
Amedai hatabadili Mfumo huo licha ya kucheza na Man United ngumu na yenye uzoefu.
Kikosi cha Ajax kinategemewa kuwa na Vijana watupu na Mchezaji pekee mwenye Umri zaidi ya Miaka 25 ni Lasse Schone.
Man United wataingia Mchezoni wakimkosa Beki wao Eric Bailly ambae alipewa Kadi Nyekundu kwenye Nusu Fainali na Velta Vigo na hivyo Kufungiwa.
Piam Straika wao mahiri, Zlatan Ibrahimovic, Mwenyeji wa Sweden aliewafungia Man United Bao 5 kwenye Mashindano haya, hayupo akijiuguza Goti lake.
Majeruhi wengine wa Man United ni Luke Shaw, Marcos Rojo na Ashley Young.
Ajax, ambao walimaliza Nafasi ya Pili kwenye Ligi ya kwao, watamkosa Fulbeki wao wa Kushoto Nick Viergever ambae yupo Kifungoni.
No comments:
Post a Comment