MABINGWA WAPYA wa Spain Real Madrid wamemsaini Vinícius Júnior kutoka Flamengo ya Brazil kwa Dau la Pauni Milioni 39.6.
Tineja huyo amekichezea Kikosi cha Kwanza cha Flamengo Mechi 1 tu. Inadaiwa Klabu za Barcelona na Manchester United zilitoa Ofa za Euro Milioni 30 lakini ile ya Euro Milioni 46 ya Real ndio imewini.
Vinícius Júnior alisaini Mkataba Mpya na Flamengo Wiki iliyopita na ndani yake kubadilishwa Kipengele cha Kuuzwa kwake wakati Mkataba ukiwa hai kutoka Euro Milioni 30 hadi 46 ambazo ndizo Real wamelipa.
Dili hii imemfanya Kinda huyu kuwa Mchezaji wa Bei mbaya wa Pili kununuliwa katika Historia ya Brazil baada Neymar kununuliwa na Barcelona kutoka Santos Mwaka 2013 kwa Dau la Euro Milioni 86.
Mara baada Dili ya Kijana huyu kukamilika, Real imetangaza kuwa wataanza kummiliki Mchezaji huyu kuanzia Julai 2018 akitimiza Miaka 18 lakini atabaki Flamengo hadi Julai 2019.
Vinicius ameichezea Timu ya Taifa ya Brazil ya U-17 mara 22 akipachika Bao 19.
Kwenye Ubingwa wa Nchi za Marekani ya Kusini w U-17, Vinicius ndie aliibuka Mchezaji Bora na Mfungaji Bora akipiga Bao 7.
No comments:
Post a Comment