Sam Allardyce, maarufu kama Big Sam, amejiuzulu kama Meneja wa Crystal Palace mara baada ya kuinusuru kushuka Daraja ikiwa ni Miezi Mitano tu tangu ajiunge nao.
Allardyce alijiunga na Palace Mwezi Desemba kumrithi Alan Pardew na kupewa Mkataba wa Miaka Miwili na Nusu.
Wakati huo Palace walikuwa nafasi za mkiani kwenye Msimamo wa EPL, LIGI KUU ENGLAND wakiwa Pointi 1 tu juu ya zile Timu 3 za mwisho ambazo hushushwa Daraja.
Lakini Big Sam, ambae kabla alikuwa Meneja wa Timu ya Taifa ya England kwa Gemu 1 tu na kulazimika kujiuzulu kutokana na kashfa, aliweza kuiongoza Palace ishinde Gemu 8 kati ya 21 na kujikita Nafasi ya 14 katika EPL yenye Timu 20 na hivyo kuinusuru kushushwa Daraja.
Hilo lilimfanya Big Sam, ambae ashawahi kuwa Meneja kwenye Klabu za Bolton, Blackburn, Newcastle na West Ham, kudumisha Rekodi yake safi ya kutowahi kushushwa Daraja akiwa na Klabu yeyote.
Akiongea mara baada ya uamuzi huu wa kuondoka Palace ukitangazwa, Big Sam alisema: "Sina haja kushika kazi nyingine. Nataka nifurahie maisha!"
Huyu anakuwa Meneja wa pili Wiki hii kuondoka Klabuni kwa hiari yake baada Juzi David Moyes kuamua kuondoka Sunderland ambayo imeshushwa Daraja kutoka EPL.

No comments:
Post a Comment