BUKOBA SPORTS

Tuesday, May 2, 2017

WENGER AUNGAMA, MAHASIMU WAO SPURS NI MOTO, JUMAPILI ARSENAL KUWAVAA MAN UNITED!

Arsene Wenger ameungama kuw Tottenham Hotspur wanastahili kuwa juu ya Arsenal kwenye Msimamo wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, baada ya Jana wao kufungwa 2-0 huko White Hart Lane.
Kipigo hicho kimehakikisha Kikosi cha Spurs chini ya Meneja Mauricio Pochettino sasa kitamaliza kikiwa juu ya Arsenal kwenye Msimamo wa Ligi kwa mara ya kwanza katika Miaka 22.
Baada Mechi 34 Spurs wako.Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 77 na Arsenal wapo Nafasi ya 6 wakiwa wamecheza Mechi 33 na wana Pointi 60.

Wenger ameeleza: "Tazama, Pointi ni Pointi.
Hazitoki mbinguni unazipata Uwanjani.
Nikiamini au nisiamini pengo lipo!"
Katika Miaka yake zaidi ya 20 akiwa na Arsenal, Wenger hajawahi kumaliza nje ya 4 Bora ya Ligi lakini safari hii yupo hatarini kulikosa hilo huku faraja pekee kwao ni kutinga Nusu Fainali ya FA CUP ambayo watacheza na Chelsea.
Jumapili Arsenal wataikaribisha Emirates Man United iliyo Nafasi ya 5 na ambao wako Pointi 5 mbele yao huku Man City ambao wako Nafasi ya 4 wako Pointi 6 mbele ya Arsenal.
Wenger amesema: "Ni ngumu sasa lakini ni lazima tupigane! Bado tuna nafasi 4 Bora inabidi tujikokote toka hapa na kujitayarisha kwa Gemu zetu zijazo!"

No comments:

Post a Comment