Hii ni mara ya kwanza kwa Man United kuongoza Listi hiyo katika Miaka Mitano.
Kwa mujibu wa Forbes, Barca sasa thamani yao ni £2.82bn na Real, ambao ndio walikuwa Namba Wani kwa Miaka Minne iliyopita, thamani yao ni £2.77bn.
Timu zinazofuatia ni Bayern Munich wenye £2.10bn na Manchester City, ambao sasa wameipita Arsenal, wana £1.61bn.
Timu 6 za EPL, LIGI KUU ENGLAND, zipo kwenye 10 Bora zikiungana na Man United ambazo ni Man City, Arsenal, Chelsea, Liverpool na Tottenham.
Kwa Mwaka 2015/16, Man United ilivuna Mapato ya £593m wakizizidi Barca na Real kwa zaidi ya Pauni Milioni 60.
10 BORA - KLABU ZENYE THAMANI KUBWA DUNIANI:
1) Manchester United - US$3.69bn (£2.86bn)
2) Barcelona - $3.64bn (£2.82bn)
3) Real Madrid - $3.58bn (£2.77bn)
4) Bayern Munich - $2.71bn (£2.10bn)
5) Manchester City - $2.08bn (£1.61bn)
6) Arsenal - $1.93bn (£1.50bn)
7) Chelsea - $1.85bn (£1.43bn)
8) Liverpool - $1.49bn (£1.15bn)
9) Juventus - $1.26bn (£980m)
10) Tottenham - $1.06bn (£820m)
No comments:
Post a Comment